Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah al-‘Udhma Jawadi Amoli katika maandishi yake amezungumzia suala la rafiki na mwenza mwenye hekima, na amesema:
«وَ احْذَرْ صَحَابَةَ مَنْ یَفِیلُ رَأْیُهُ»
Amesema: uwe mwanafunzi wa Hawza au wa chuo kikuu, chagua rafiki na mwenza mwenye busara. Huna haja ya kufanya urafiki wa karibu na mtu asiye na kipawa, asiye na ufahamu mzuri, asiye na uelewa wa kina, asiye na kumbukumbu nzuri, na ambaye ni dhaifu katika kutoa maoni.
Urafiki wa kijamii kwa kiwango cha jumla si jambo baya, kiasi cha kwamba kila Mwislamu awe na uhusiano mzuri na Mwislamu mwenzake; lakini unapochagua rafiki wa karibu, ni lazima awe na kipawa na akili salama.
«وَ احْذَرْ صَحَابَةَ مَنْ یَفِیلُ رَأْیُهُ وَ یُنْکَرُ عَمَلُهُ»
Yaani: yule ambaye hana elimu sahihi, hana vipawa vizuri, wala hana matendo mema; huna sababu ya kumfanya awe rafiki yako wa karibu nawe.
«فَإِنَّ الصَّاحِبَ مُعْتَبَرٌ بِصَاحِبِهِ»
Hakika rafiki hutambulika kwa rafiki yake, na mtu hutambulika kwa watu anaoshirikiana nao.
Darsa ya Maadili – 9 Azar 1396 H.S. (30 Novemba 2017 Miladi)
Maoni yako