Kwa mujibu wa ripoti ya idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji, Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf, katika khutba za Swala ya Ijumaa alizotoa katika Husseiniyya Adhimu ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf, alisema: Gazeti rasmi “Al-Waqa’i‘ Al-‘Iraqiyya”, lenye jukumu la kuchapisha maamuzi yote ya serikali, limechapisha sheria kuhusu kufungiwa mali za magaidi wanaoshirikiana na Daesh; miongoni mwao likiwataja Hezbollah ya Lebanon na Wahouthi wa Yemen. Jambo hili ni la ajabu na halikubaliki kabisa; inawezekanaje marafiki wakageuka kuwa maadui, na maadui wakageuka kuwa marafiki?
Aliongeza kusema: Ingawa serikali imetangaza kwamba uamuzi huo ulikuwa kosa lisilo la kukusudiwa, sisi tunaamini kuwa kosa hilo halisameheki, na lazima lifanyiwe uchunguzi na waliohusika wawajibishwe na kupewa adhabu.
Trump anapaswa kuhukumiwa katika mahakama za kimataifa, si kupewa Tuzo ya Amani ya Nobel
Imamu wa Ijumaa wa Najaf Ashraf alisisitiza kuwa: Miongoni mwa mambo ya kushangaza zaidi ni kwamba Trump anadai serikali ya Iraq imependekeza apewe Tuzo ya Amani ya Nobel! Ilhali huko Palestina mashahidi elfu sitini wameuawa, naye ndiye msaidizi mkuu wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, Syria, Yemen na Iran; kwa hivyo, kinachomstahikia Trump ni kuhukumiwa kimataifa, si kupewa pongezi.
Katika sehemu nyingine ya khutba yake, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji aliwashukuru wanajeshi wa Hashd al-Sha‘abi ambao kutoka na juhudi zao waliweza kuikarabati na kuijenga upya Hospitali ya wagonjwa wa akili ya Al-Rashad jijini Baghdad, iliyokuwa inakaribia kuporomoka.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qabanji pia aligusia kumbukumbu ya kufariki Bibi Ummul-Banin (a.s.), na kusema: Mwanamke huyu mkubwa alifanya jihadi katika nyanja mbili; jihadi ya kujitolea kikamilifu — pale alipotoa mali yake yote, yaani watoto wake wanne, kwa ajili ya Imam Hussein (a.s.). Na jihadi ya kuhifadhi na kuendeleza harakati ya Imam Hussein (as), pale alipokuwa kila siku akifanya majlisi za maombolezo kwa ajili ya wanawe waliouawa katika njia ya haki, ili kumbukumbu ya Ashura na lengo la mapinduzi ya Imam Hussein (a.s.) viendelee kuishi.
Maoni yako