Jumanne 2 Desemba 2025 - 14:50
Ili Kuokoka na Majuto ya Siku ya Kiyama Tufanye Nini?

Hawza/ Kila wakati unaopita bila kumkumbuka Mwenyezi Mungu, huacha majuto marefu; na kumbukumbu hii si kwa ulimi pekee, bali lazima ionekane na idhihirike pia katika vitendo.

Shirika la Habari la Hawza - Kuhusiana na umuhimu na thamani ya dhikri na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, inatosha tu kwamba Qur’ani Tukufu inasema:

﴿فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ﴾

Basinikumbukeni Mimi, nami Nitawakumbuka nyinyi. (1)

Sherehe:
Moja ya mambo yaliyopewa umuhimu mkubwa sana katika mafundisho ya dini ya Uislamu ni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kushughulika na dhikri Yake. Dhikri na kumbukumbu ambayo hata ikisahaulika kwa muda mfupi tu kwa sababu ya kughafilika, huleta majuto marefu.

Kama alivyosema Mtume Muhammad (s.a.w.w):

«ما مِن ساعَةٍ تَمُرُّ بِابن آدَمَ لَم یُذکَرِ اللهُ فیها إلّا حَسِرَ عَلَیها یَومَ القیامَةِ»

Hakuna hata saa moja inayompita mwana damu ambayo hakumkumbuka Mwenyezi Mungu ndani yake, isipokuwa ataijutia saa hiyo Siku ya Kiyama. (1)

Hakika inapozungumziwa dhikri na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, haikusudiwi dhikri ya ulimi pekee, bali dhikri ya vitendo pia. Dhikri inayoishi na kuenea katika maisha ya mwanadamu na kudhihirika katika nyanja zote za maisha yake. Dhikri inayoyafanya maisha yake yote yapambike kwa rangi ya uungu.

Na hakika ikiwa mja atauunganisha ulimi na moyo wake pamoja na kupambwa na dhikri ya vitendo, ndipo Mwenyezi Mungu naye humkumbuka mja huyo: «أَذْكُرْكُمْ».

Mwenyezi Mungu ambaye ni Mmiliki wa mbingu, Mmiliki wa ardhi, na Mmiliki wa Siku ya Kiyama, humkumbuka mja huyo.

Wakati ambapo katika uwanja wa Mahshar kuna watu fulani ambao kwa sababu ya kughafilika kwao duniani juu ya Mwenyezi Mungu na kumkumbuka yeye, watafufuliwa wakiwa vipofu. (3)
Mwenyezi Mungu atakuwa nuru na taa ya kumuongozea mja huyu, atamtoa katika upweke na hofu ya Kiyama na atamwekea sababu za kupata furaha ya milele; kwa kuwa Mwenyezi Mungu kamwe hakeuki ahadi Yake. (6)

Rejea:
1. Surat Al-Baqara, Aya ya 152.
2. Kanzul-‘Ummal, Hadithi Na. 1819.

٤. ﴿وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى﴾  طه: 124

٥. ﴿لَا يُخْلِفُ اللَّهُ وَعْدَهُ﴾ الروم: 6

Imeandaliwa katika Kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha