Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza - marehemu Ayatollah al-‘Udhmaa Bahjat alijibu swali la mmoja alie uliza kuhusu namna ya kupata unyenyekevu moyoni katika Swala kwa maneno yafuatayo:
Swali la muulizaji:
Marehemu Ayatollah Qadhi (ra) alikuwa amesema kuwa mtu yeyote anayeshikamana na kuswali mwanzo wa wakati hufikia daraja za juu za kiroho; je, pia aliweka sharti la hudhuri moyoni na unyenyekevu au la?
Jibu la marehemu Ayatollah al-‘Udhmaa Bahjat:
Kuswali mwanzo wa wakati kwenyewe huleta unyenyekevu moyoni. Kushikamana na jambo hili kunamaanisha; yaani mtu aache shughuli zake na aelekee kwenye Swala — kufanya hivyo pekee huleta tayari unyenyekevu moyoni.
Kwa mfano, leo huleta kiasi fulani cha unyenyekevu moyoni. Mwishowe utaona kuwa kesho, kesho kutwa na siku zinazofuata, unyenyekevu moyoni katika Swala unaongezeka siku baada ya siku
Maoni yako