Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, msemaji wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) siku ya Ijumaa alitangaza kuwa tangu kuanza kwa kusitishwa mapigano kati ya Hamas na Israel, watoto 67 ndani ya Ghaza wamefariki dunia. Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Geneva, aliongeza kuwa takwimu hizi zinamaanisha kuwa wastani wa watoto wawili wa Kipalestina huchukuliwa maisha yao kila siku katika matukio yanayohusiana na vita hivi.
Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) lilitangaza kuwa tangu kuanza kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza, takriban watoto 67 wameuawa katika matukio yanayohusiana na vita kati ya Hamas na Israel.
Ricardo Pires, msemaji wa UNICEF, aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa: “Makumi ya watoto wengine wamejeruhiwa. Hii ina maana kwamba tangia kuanza kutekelezwa kwa kusitishwa mapigano, kwa wastani karibu watoto wawili wamefariki kila siku.”
Katika muktadha huu, “Israel” tangia tarehe 7 Oktoba 2023 — kwa msaada wa Marekani na Ulaya — imekuwa ikitekeleza mauaji ya halaiki katika Ukanda wa Ghaza, yanayojumuisha kuua, kusababisha njaa, uharibifu, kuwafukuza watu makwao na kuwakamata. Hatua hizi zinaendelea licha ya wito wa kimataifa na maagizo ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya kusitisha vitendo hivyo kupuuzwa.
Mauaji haya ya halaiki yamesababisha zaidi ya Wapalestina 240,000 kupata shahada na majeruhi, huku wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake. Zaidi ya watu 11,000 pia hawajulikani walipo, mbali na mamia ya maelfu ya wakimbizi na baa la njaa lililochukua maisha ya wengi, hasa watoto. Aidha, uharibifu mkubwa umefanyika, na miji mingi ya Ukanda huu imetoweka kabisa kwenye ramani.
Maoni yako