Ijumaa 21 Novemba 2025 - 23:30
Mjumbe wa Kambi ya Muqawama: Wazayuni wamelijaribu taifa letu tangu 1948 hadi leo, lakini hawajavunja azma yake

Hawza/ Husein Jushi alisema: Tunaitaka serikali iitishe Kamati ya Utaratibu (Mekanizimu) ili kusitisha uvamizi dhidi ya raia na iwasilishe malalamiko kwa Baraza la Usalama.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Husein Jushi, mwanachama wa Kambi ya Muqawama, katika mahojiano na Redio al-Nur, alieleza kuwa adui Muisrael daima amekuwa mstari wa mbele katika kutenda jinai dhidi ya Walebanon, na anaamini kwamba kufikia malengo yake ya uvamizi kunategemea mantiki ya vitisho, mauaji na umwagaji damu. Anataka kupitia mashambulio yake ya kuendelea hata baada ya kusitisha mapigano, kukwepa utekelezaji wa Azimio 1701, na anatamani kwamba kupitia shinikizo, vitisho na kuua, aweze kulazimisha “mkataba wa amani” na Lebanon — sera inayoungwa mkono na Marekani. Anaamini kwamba taifa letu litachoka, lisalimu amri na liache kuungana na Muqawama.

Akaongeza kuwa: Wanajaribu kuiweka Lebanon katika chaguo mbili ambazo zote ni kwa hasara ya Lebanon. Chaguo la kwanza ni jeshi kunyang’anya kwa nguvu silaha za Muqawama kwa kisingizio cha kuzuia Walebanon kugombana — jambo ambalo si kwa maslahi ya Lebanon. Chaguo la pili ni kuitisha kwamba Israel itaiingiza Lebanon vitani, hali ya nchi iwe ngumu, kisha lawama ibebeshwe serikali ya Lebanon, jambo litakalosababisha hasara na madhara. Huu ndio mtindo wa adui Muisrael na Mmarekani — ubabe na mabavu yanayotumiwa kwa kigezo kwamba kutokana na mabadiliko ya eneo, hususan Syria, hili ni dirisha lao la kutawala eneo.

Jushi akaendelea: Nadhani Waisrael wamelipima taifa letu tangia 1948 hadi leo kupitia mauaji, vitisho na uvamizi wa 1982, 1993, 1996, 2006 na 2024. Lakini hawajawahi kuivunja azma ya taifa letu; na hawatafanikiwa. Hata hivyo, jambo kuu ni kwamba kamati ya usimamizi wa kusitisha mapigano ina wajibu — iwe Marekani au Ufaransa, hata kama Marekani ni mshirika wa wazi — lakini pia serikali ya Lebanon, iwe rais au baraza la mawaziri, imekubali jukumu la kuwalinda Walebanon, hivyo wana wajibu. Waache waje wabebe jukumu hili, kwa kuwa heshima ya serikali ipo majaribuni leo.

Mjumbe huyo wa Kambi ya Muqawama akaongeza: Serikali ina chaguzi nyingi lakini haitumii chochote. Kwa mfano: je, kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita, ni mara ngapi imewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama? Pia tuna serikali, taifa, Muqawama, uwezo na fursa za kidiplomasia, lakini havitumiki. Na muhimu zaidi, pale serikali inapodai peke yake kuwa na silaha, wakati uvamizi wa kila siku wa Israel unaendelea na adui anakalia ardhi yetu, basi sisi kwa kujua au kutokujua tunakuwa tunamsaidia adui.

Alilaani vikali mashambulio haya ya kigaidi yaliyosababisha wananchi wengi kuyahama makazi yao, na ambayo leo asubuhi yamewajeruhi wanafunzi kadhaa waliokuwa wakielekea shuleni kwa basi, ukiukaji wa wazi wa uhuru na mamlaka ya Lebanon.

Jushi alitoa wito kwa kusema: Serikali iitishe Kamati ya Utaratibu (Mekanizimu) ili kusitisha uvamizi dhidi ya vijiji vinavyo kaliwa na raia, na iwasilishe malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili adui akemeewe na mashambulio dhidi ya raia yakomeshwe.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha