Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Ali Fadhlallah, kupitia mawasiliano ya simu, sambamba na kutoa mkono wa pole, amelaani mauaji yaliyofanywa na Israel katika kambi ya Ain al-Hilweh.
Alizungumza kwa simu na Dkt. Nadī Yusuf, mke wa Mkurugenzi wa Shule ya al-Mansūriy, na kutoa salamu zake za rambirambi kwa shahada ya mume wake, mwalimu Muhammad Shuweikh, aliyeuawa katika shambulio la Kizayuni.
Hujjatul-Islam Fadhlallah alisisitiza thamani ya kimalezi na hadhi kubwa ya shahidi huyu, na akaashiria kwamba adui wa Kizayuni kupitia hujuma hii analenga kuufuta ukweli na historia, na kudhuru vipengele vyote vya kusimama kidete na uimara, hususan sekta ya elimu na malezi.
Aidha, alizungumza kwa simu na “Abir Sharara”, mwandishi wa habari, na kutoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha ndugu yake Hassān.
Sayyid Fadhlallah pia alitoa mkono wa pole kwa familia ya Zuhayr al-Khatīb, mbunge wa zamani wa bunge, na akaashiria kuwa marehemu alikuwa sura muhimu ya kitaifa na Kiarabu, na akasifu nafasi yake ya kisheria, kitaifa na kimapambano katika kulilinda taifa dhidi ya tamaa za Kizayuni.
Kwa upande mwingine, Imamu wa Ijumaa wa Beirut alilaani vikali mauaji ambayo adui wa Kizayuni ameyafanya dhidi ya watu wasio na hatia katika kambi ya Ain al-Hilweh na kusababisha kuwawa na kujeruhiwa idadi ya watu.
Alisisitiza kwamba hujuma hii inaonesha unyama na usaliti wa adui huyu, na jitihada zake zinazoendelea za kuharibu vipengele vya uthabiti, uimara na irada ya taifa la Palestina ili kuwakengeusha waachane na haki yao ya kurejea katika ardhi ya mababu zao.
Maoni yako