Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Alireza A’rafi, Mkurugenzi wa Hawza nchini Iran, katika kongamano la wanafunzi wapya wa Hawza ya Qom lililofanyika leo kabla ya adhuhuri katika ukumbi wa Baqi’ ndani ya Msikiti Mtukufu wa Jamkaran, huku akiwapongeza vijana kwa kuchagua njia hiyo, alianza hotuba yake kwa tafsiri ya aya ya 46 ya Suratu Saba:
{قُلۡ إِنَّمَاۤ أَعِظُكُم بِوَ حِدَةٍۖ أَن تَقُومُوا۟ لِلَّهِ مَثۡنَىٰ وَفُرَدَىٰ}“Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili-wawili na mmoja-mmoja”
Mkurugenzi wa Hawza aliielezea aya hii tukufu kuwa “miongoni mwa aya bora na zenye fahari ndani ya Qur’ani Tukufu” na akaongeza kuwa: Aya hii ni bahari ya maana tukufu. Miongoni mwa mada mbalimbali, nimeichagua aya hii ili nyinyi wapendwa, mwanzoni mwa safari ndefu na tukufu mliyoichagua, muifanye kuwa taa ya kuwaongoza.
Kufufua upya mazingira ya kisiasa na kijamii ya mwaka 1326 (Hijria Shamsia) na kumbukumbu ya kudumu
Ayatollah A’rafi akiendelea, kunesha taswira ya mazingira ya kihistoria ya Iran mwaka 1326, alikumbusha: Kipindi hiki kilikuwa ni miaka michache baada ya kuanguka kwa Reza Khan na mwanzoni mwa utawala wa Muhammad Reza Pahlavi; zama ambazo mazingira yake yalijaa mapambano dhidi ya dini, thamani za kimungu, na mizizi ya utambulisho wa Kiislamu na kitaifa wa nchi. Katika eneo hili pia kulikuwa na mawimbi ya shinikizo kutoka kwa nguvu za nje, hasa Uingereza, kwa lengo la kudhoofisha dini na kuangamiza imani za kimungu.
Mwanzo wa kumbukumbu ya Imam Khomeini (r.a) kwa aya isemayo: “Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu
Mkurugenzi wa Hawza Iran, akielezea uwepo wa Imam Khomeini (r.a) mjini Yazd katika kipindi hicho, alisema: Wakati huo, marehemu Waziri alikuwa ameanzisha maktaba muhimu na ya kihistoria ya Waziri huko Yazd, na alikuwa akichukua kumbukumbu ya maandishi kutoka kwa kila mgeni. Imam Khomeini (r.a) pia katika mwaka 1326 shamsia, aliandika kumbukumbu ya ukurasa mmoja katika maktaba hiyo, ambayo matini yake kamili imo katika Sahifa ya Imam.
Mkurugenzi huyo wa Hawza alisema: Imam Khomeini (r.a) alianza kumbukumbu yake kwa aya hii. Aya ambayo takriban miaka 14 au 15 kabla ya kuanza kwa mapinduzi, na kabla ya yeye kubeba jukumu la uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu na uimamu, ilikuwa mhimili wa mawaidha yake ya kimaadili na uchambuzi wake wa kimtazamk juu ya mustakabali.
Ayatollah A’rafi akaongeza: Chini ya kumbukumbu hiyo, Imam alitoa nasaha za kimaadili zenye thamani na akafanya dondoo za kiufanisi kuhusu mustakabali wa harakati na mabadiliko yaliyokuwa yakionekana katika upeo wa fikra zake; kana kwamba misingi ya Mapinduzi ya Kiislamu ilikuwa imejikita katika nafsi yake miaka mingi kabla ya kutokea kwake.
Uchambuzi wa muundo wa aya “Sema: Sema: Mimi nakunasihini kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu,...”
Mjumbe wa Baraza la Uongozi wa Hawza, kisha akaelezea muundo wa aya hiyo akisema: Mwanzoni mwa aya imekuja amri “Sema”. Ingawa Qur’an yote ni wahyi wa Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w) amepewa jukumu la kufikisha yote, lakini katika baadhi ya aya, neno “Sema” hutumika ili kuonesha msisitizo, ubainifu na umuhimu maalumu wa ujumbe. Baada ya “Sema” linakuja neno “Hakika” (Innama), ambalo lina maana ya upekee; yaani ujumbe unaofuata ni maalumu na wa kipekee.
Mkurugenzi wa Hawza aliendelea: Kisha Mwenyezi Mungu anasema: “Ninawasihini kwa moja tu”. Hii ni hakika ya kushangaza, kwa sababu Qur’an yote imejaa mawaidha na miongozo; lakini miongoni mwa yote hayo, Mwenyezi Mungu anachagua ujumbe mmoja kuwa ni msingi na mhimili. Ujumbe huu muhimu sana ni kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa pamoja na mmoja mmoja, na baada ya hapo mfikiri. Huu ndio muhtasari wa harakati ya Manabii, Mawalii na harakati zote za kimungu.
Kusimama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu: Msingi wa mabadiliko ya mtu binafsi na jamii
Mjumbe wa Baraza Kuu la Hawza, akieleza upeo wa maana ya kusimama kwa ajili ya Allah, alisema: Kusimama kwa ajili ya Mungu ni harakati iliyo na mizizi, inayotokana na nia safi, ufahamu, fikra na kutegemea imani. Ni kusimama kunakomtoa mtu kutoka katika utegemezi, dhana ya kumilikiwa, na hofu, na kumweka katika njia ya haki. Aya hii inatufundisha kwamba kila mabadiliko makubwa huanza kwa kusimama kwa ajili ya Mungu; iwe katika eneo la kutakasa nafsi, shughuli za kijamii, au jihadi ya kielimu na kiutamaduni.
Maoni yako