Jumamosi 1 Novemba 2025 - 06:40
“Mpango wa kusitisha vita vya Ghaza” ni mchezo wa Trump katika ardhi ya Netanyahu

Hawza/ Hujjatul-Islam Sayyid Sadiqi Husayni katika hotuba yake alisema: Trump kwa kuwasilisha mpango wa utata kuhusu mgogoro wa Ghaza, amefanya kazi kwa manufaa ya Netanyahu, na watu wa Ghaza walioko chini ya vikwazo bado wanaendelea kushambuliwa.

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Sadiq Husein katika hotuba yake alisema: Trump, ili kujitangaza duniani, alielekea Mashariki ya Kati. Tumeona kuwa alijaribu kujiingiza katika vita vya Ukraine na hata akataka kujitangaza kuwa mfalme, lakini jambo pekee alilolipata lilikuwa ni maandamano ya mamilioni ya wananchi wa Marekani dhidi yake.

Vita vya Ghaza vimeleta shinikizo kubwa la kiuchumi na kisiasa kwa Israel na Marekani. Kwa hivyo, Trump alitoa pendekezo la mpango wa kuondokana na shinikizo hilo, ambao kwa hakika ulikuwa ni wa manufaa kwa mshirika wake Netanyahu pekee. Wakati huo huo, tunaona kwamba mpango huo hauna faida yoyote kwa watu wa Ghaza wanaokumbwa na njaa, kwani licha ya pande zote kukubali usitishaji wa vita, utawala wa Kizayuni bado unaendelea na mashambulizi na mzingiro wa Ghaza.

Chanzo: Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu ya Kiislamu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha