Jumatatu 20 Oktoba 2025 - 22:48
Muungano wa Kidini Chini ya Uongozi wa Mtume wa Uislamu (s.a.w.w)

Hawza/ Naibu wa masuala ya kimataifa wa hawza amesema kuwa; maandalizi maalumu ya maadhimisho ya miaka 1500 tangu kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni fursa adhimu kwa ajili ya kuikuza fikra ya Mtume na kutatua migogoro ya ulimwengu wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa  Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Sayyid Mufid Husayni Kuhsari, katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, alisema: “Maadhimisho haya ya miaka elfu moja na mia tano tangia kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) yamekuja sambamba na mabadiliko muhimu ya kihistoria na hatima ya ulimwengu wa Kiislamu. Mabadiliko makubwa yamejitokeza katika upande wa muqawama huko Ghaza. Leo, suala la Palestina limevuka mipaka ya nchi za muqawama na kuwa ni tatizo la dunia nzima. Leo hii, maelfu ya mikusanyiko, shughuli na matukio yameandaliwa katika nchi za Kiislamu na hata za Magharibi kuhusiana na suala la Ghaza.”

Akaongeza kuwa: “Chuki dhidi ya Israel na taasisi za kimataifa ambazo zimenyamazia uhalifu wa utawala huo zimekuwa mada kuu duniani. Leo dunia imehama kutoka mfumo wa dunia ya upande mmoja na kuelekea dunia yenye pande nyingi, ambapo nguvu za kijeshi, kisiasa, kitamaduni na kiuchumi ziko katika mchakato wa kuibuka na kubadilika.”

Naibu huyo wa Kimataifa wa hawza alisema: “Katika hatua hii muhimu ya kihistoria, ni jukumu la ulimwengu wa Kiislamu na wanazuoni wake kutoa tafsiri mpya ya utu wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na mafundisho ya sunnah na sirah yake tukufu. Tukio hili, katika mazingira haya ya kihistoria, linaweza kutusaidia katika mchakato wa kujenga umma mmoja na kuunda ustaarabu wa Kiislamu.”

Hujjatul-Islam Kuhsari aliongeza: “Kuzungumzia na kuchunguza utu wa Mtume (s.a.w.w) katika ngazi fulani kunaweza pia kuwa na malengo ya kitaifa, kwa kuwa kunachochea mjadala mpya kuhusu nafasi ya Mtume miongoni mwa tabaka zote za nchi yetu. Tunapaswa kumfahamu zaidi Mtume kwa mtazamo wake wa kijumla na wa kiustaarabu; pia tuelewe vipengele vya utu wake, siasa zake, utamaduni wake, uongozi wake, malezi yake, na uchumi wa maisha yake. Tunatumai fikra mpya na uzalishaji wa maarifa yenye thamani utafanyika katika nyanja hizi.”

Kuimarisha Wazo la Urithi Mkubwa wa Mtume (s.a.ww.)

Akaendelea kusema: “Leo tunamiliki urithi mkubwa wa kielimu unaojumuisha maelfu ya vitabu, makala na utunzi. Tunatumai kuona harakati kubwa katika mchakato wa kuibua fikra na mijadala kutokana na kazi hizo. Bila shaka, hadhi tukufu na ya kipekee ya Mtume (s.a.w.w) inahitaji kufanyike tafiti na nadharia mpya kumhusu yeye, na tunatarajia mwaka huu tuone upeo mpya wa tafakuri na utamaduni unaozunguka utu wake. Hili linaweza pia kuchangia kuimarisha umoja wa kitaifa, baina ya ndugu zetu Ahlus-Sunnah na wafuasi wa madhehebu ya Ahlul-Bayt.”

Hujjatul-Islam Kuhsari alisisitiza: “Katika uwanja wa ulimwengu wa Kiislamu, mchakato huu wa kujenga fikra unaweza kuongeza mshikamano wa Waislamu. Tunakabiliwa na changamoto na madhara makubwa katika juhudi za kuunda umma mmoja wa Kiislamu, lakini hakika tunaweza, chini ya kivuli cha utu wa Mtume (s.a.w.w) na mafundisho yake, kufungua upeo mpya wa umoja thabiti na imara zaidi.”

Athari za Kimadhehebu na Kimataifa za Kumuadhimisha Mtume (s.a.w.w)

Akaongeza kusema:b“Kadhalika, katika uwanja wa mahusiano ya kidini duniani, tunaweza kunufaika mno kutokana na utu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Hadhi yake tukufu, pamoja na upeo wa kielimu, kimijadala, kimaadili, na fikra za heshima, haki, maadili, izza na rehema vilivyomo ndani yake, ni mhimili mkuu unaoweza kuziunganisha dini zote na falsafa mbalimbali duniani. Tunaamini kwamba chini ya kivuli cha utu huu wa kimataifa na wa mbinguni, tunaweza kuunda kiungo kipya cha kimataifa kinachowaunganisha wanadamu wote.”

Naibu huyo wa Kimataifa wa hawza aliendelea kusema:  “Katika uwanja huu, hatupaswi kutupitilia mbali baadhi ya maelezo duni na yasiyo kamili yaliyotolewa kumhusu Mtume (s.a.w.w), bali tunapaswa kuyasahihisha na kuyarekebisha. Inatupasa pia kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu na upotoshaji unaoenezwa duniani. Tunatarajia kuwa kwa njia ya kielimu, kimaarifa na kitamaduni, mwaka huu utakuwa ni nukta muhimu katika historia ya ulimwengu wa Kiislamu, ambapo tutachukua hatua madhubuti kwa kutumia utu wa Mtume (s.a.w.w) na malengo yake ya kiutume katika kuujenga umma mmoja.”

Mipango ya Kielimu, Kimaudhui ya Kimataifa katika Kumuenzi Mtume (s.a.w.w)

Akaendelea kusema: “Katika nyanja hii, zimepangwa programu za kielimu, kiutamaduni, kimaarifa na za kimataifa. Matukio ya kitaifa yameandaliwa ndani ya taasisi za hawza. Leo, Waislamu wote, kwa sababu ya upendo na mapenzi yao kwa Mtume (s.a.w.w), bila shaka wanaweza kuandaa kwa hiari yao shughuli mbalimbali za kumuadhimisha. Haimaanishi kwamba shughuli zote lazima ziwe za kiserikali au za kitaasisi. Zimepangwa pia programu zitakazowawezesha wampendao Mtume (s.a.w.w) katika nyanja zote kuonesha upendo na heshima zao kwa utu wake mtukufu.”

Hujjatul-Islam na Mujtahid Husayni Kuhsari aliweka bayana: Mbali na aina mbalimbali za diplomasia za wanazuoni pamoja na diplomasia za kielimu na kitamaduni, pia kuna diplomasia za vijana, za sanaa, za wanawake na zile za michezo n.k. ambazo zinaendelea kuchezewa katika ulimwengu wa Kiislamu; kwa hivyo, kwa kuamsha na kuendesha aina hizi tofauti za diplomasia tunaweza kuchukua hatua za msingi katika kuinua hadhi ya Mtume (s.a.w.w) na kuiboresha, mwingiliano wa Jamhuri ya Kiislamu na nchi mbalimbali. Zaidi ya hayo, hata zaidi ya mipaka ya dunia ya Kiislamu tunaweza kusukuma mwamko wa kuinuliwa kwa nafasi ya Mtume katika ngazi za kidini na kimataifa chini ya sura ya utu wake mtukufu.

Aliongeza kuwa: katika muktadha huu inawezekana kushirikishwa mashirika na taasisi za kimataifa kama Mkutano wa Nchi za Kiislamu pamoja na vikao vingine vinavyoaminika katika ulimwengu wa Kiislamu, ikiwemo Al-Azhar, vyuo vikuu vya Kiislamu na vikao vya fiqh na dini; kwa kushirikiana na taasisi hizo tunaweza kuandaa shughuli na mipango bora zaidi. Tayari shughuli mbalimbali zimepangwa, na kupitia uwezo na nyenzo za kimataifa za umma wa Kiislamu inawezekana kuchukuliwa hatua za dhati za kuimarisha hadhi ya ulimwengu wa Kiislamu na kuendeleza njia za kutatua changamoto za eneo hili kwa ufanisi zaidi.

Hujjatul-Islam Husayni Kuhsari alibainisha: kutatua changamoto na migogoro ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na suala la Palestina na Ghaza, kunaweza kufuatiliwa kwa nguvu kubwa zaidi chini ya kaulimbiu moja; tunatumai kuwa mwaka huu tutaweza kuchukua hatua za msingi za kutatua matatizo yaliyopo katika ulimwengu wa Kiislamu na kuchukua hatua za kujaribu kuondoa utawala wa Kizayuni.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha