Jumanne 5 Agosti 2025 - 20:48
Siri ya Maisha Marefu na Kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa Kauli ya Ayatullah Haqqeshenas

Hawza/ Ayatullah Haqqeshenas (ra) alisisitiza kwamba kuwahudumia watu na kuwafanyia ihsani maskini, wahitaji na yatima, hakusababishi tu kuongezeka kwa maisha, bali pia ni sharti muhimu kwa ajili ya safari ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kuingia katika rehema Yake.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Haqqeshenas (ra) kwa maneno yenye kupenya, aliweka wazi kuwa kuwahudumia watu si jukumu tu, bali ni njia ya kuongeza maisha na kumkurubia Mwenyezi Mungu.

“Maisha yenu yataongezeka kutokana na kuwahudumia watu, uwepo wenu katika safari ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu unategemea ni kwa kiwango gani mnawafanyia ihsani watu wa jamii, na hili liko juu ya mambo yote.

Ikiwa kwa mlango wa rehema ya Mwenyezi Mungu mnakusudia kuingia, basi mnapaswa kutumia kiasi cha mali na kuwasaidia maskini, wahitaji na yatima.”

Chanzo: "Rahnama-ye Suluk" (Mwongozo wa Tabia), uk. 69.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha