Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ghazi Hanina, siku ya Alhamisi tarehe 22 Khordad (sawa na Juni 12), katika mkutano wa kimataifa wa “Ghadir na Mapambano” uliofanyika katika Ukumbi wa Noor, Mashhad, alizungumzia nafasi ya Ghadir katika Umma wa Kiislamu na akaeleza kuwa Ghadir ni chimbuko la umoja, heshima na mapambano ya Umma wa Kiislamu dhidi ya mabeberu wa kimataifa.
Sheikh Hanina alisisitiza kuwa Ghadir si mali ya Mashia pekee, bali ni siku kubwa ya Kiislamu inayomhusu Umma wote. Alisema kuwa Mtume Mtukufu (saw) katika siku hiyo alimtangaza wazi Amiru al-Mu’minin Ali (as) kuwa ni kiongozi na khalifa wa baada yake, na hivyo kuufafanulia Umma njia ya uongofu. Kwa mujibu wa maelezo yake, Khalifa wa Pili alilitaja bayana tukio la Ghadir kama siku ya idi na akasema kuwa ni sababu ya izza ya Umma wa Kiislamu.
Akiendelea kufafanua, alisema kuwa; suala la uongozi wa Amiru al-Mu’minin Ali (as) si jambo la mabishano ya kimadhehebu, bali ni suala lililo juu ya tofauti hizo. Alieleza kuwa mapenzi kwa Ahlulbayt (as) yamesisitizwa na madhehebu yote ya Ahl al-Sunna, na hata Ahmad bin Hanbal amepokea katika vyanzo vyake kuwa Mtume alisema: “Ali ni mgawaji wa Pepo na Moto.” Kwa mtazamo wake, haya yanaonesha kuwa upendo kwa Ali (as) ni kigezo cha imani na unafiki.
Maoni yako