Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, kwa mujibu wa kauli ya mhandisi Muntadhar Sw'alih, nakala hii ya Qur’ani Tukufu imeandikwa na kupangwa kikamilifu kutokana na jitihada za wabunifu wa picha na wasanii wa Iraq. Nakala hii ya Qur’ani imechapishwa kwa maandishi ya alfabeti ya Madina kwa hati ya ‘Uthmān Twāhā.
Mhandisi Sw'alih alisisitiza kuwa Qur’ani hii imezalishwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kabisa ya uchapishaji, jambo lililosababisha ipatikane nakala yenye ubora wa hali ya juu, inayoonesha utukufu wa maneno ya Mwenyezi Mungu na pia kuonyesha ustadi wa kisanii wa wataalamu wa Iraq.
Mafanikio haya yanawakilisha hatua muhimu ya kihistoria katika sekta ya uchapishaji wa madhehebu nchini Iraq. Aidha, ni mafanikio chanya katika kufanikisha lengo la kueneza utamaduni wa Qur’ani na kuhifadhi utambulisho wa Kiislamu, jambo ambalo linachukuliwa kama moja ya malengo makuu ya Haram ya Imamu Hussein (as).
Maoni yako