Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hadhrat Imam Muhammad Baaqir (as), ambaye jina lake ni Muhammad bin Ali bin al-Husayn, jina la laqab yake ni “Baaqir”. “Baaqir” lina maana ya mchimbuaji. Mtukufu huyu aliitwa “Baaqir al-‘Ulūm” yaani mchimbuaji wa elimu zote.
Mwanamume mmoja Mkristo, kwa dhihaka na kejeli, aligeuza neno “Baaqir” na kulitamka kama “Baqara” yaani ng’ombe, kisha akamwambia Imam: “Anta Baqara” yaani “Wewe ni ng’ombe”.
Imam bila kuonyesha maudhi wala hasira, kwa unyenyekevu kamili alijibu: “La, mimi si ‘Baqara’ (ng’ombe), mimi ni ‘Baaqir’.”
Yule Mkristo akasema: Wewe ni mwana wa mwanamke aliyekuwa mpishi tu.
Imam akasema: Hio ndio lilikuwa kazi yake. Si aibu wala fedheha yoyote.
Yule Mkristo akaendelea kusema: Mama yako alikuwa mweusi, asiye na haya, na mtu wa maneno machafu.
Imam akasema: Ikiwa madai haya unayosema kuhusu mama yangu ni ya kweli, basi Mwenyezi Mungu amsamehe na amghufirie madhambi yake; na ikiwa ni ya uongo, basi Mwenyezi Mungu akusamehe wewe kwa kutunga uwongo na kusingizia.
Kuona subira hii kubwa kutoka kwa mtu ambaye angeweza kupata kila sababu ya kumdhuru mtu ambaye si wa dini ya Kiislamu, kulitosha kabisa kuleta mapinduzi katika roho ya yule Mkristo, na kumvuta kuelekea Uislamu.
Yule Mkristo baadaye akasilimu.
Chanzo Dāstān-e Rāstān, Juzuu ya 1, uk. 48
Maoni yako