Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, filamu hii, yenye jina “Khamenei”, ni kazi ya kituo cha Al-Manar Lebanon na inajumuisha sehemu nane, ambapo Ayman Zughayb ndiye mwandishi wake. Filamu hii inaangazia kipindi cha utotoni na ujana wa Imamu Khamenei, mahali alipoishi, alikokulia na kukomaa kifikra na kimalezi.
Pia, filamu hii inaeleza kuhusu nasaba na historia ya babu wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya kiislamu katika maeneo mbalimbali kama vile Iraq, Iran, Hazaweh, Tafresh, Tabriz na Mashhad.
Filamu hii pia inaonesha historia ya elimu yake, masomo ya Hawza (vyuo vya kidini), pamoja na harakati zake dhidi ya utawala wa kidhalimu wa wakati huo, maisha yake ya gerezani na maeneo aliyopelekwa uhamishoni.
Maoni yako