Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, maulamaa wakubwa wa Bahrain wametoa tamko la pamoja huku wakilaani vikali uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza, walieleza wasiwasi wao kuhusu kuongezeka kwa mauaji ya raia wakati ambapo dunia imeendelea kukaa kimya.
Wamesema kuwa vikosi vya uvamizi vya Kizayuni vimendelea kuwaua, kuwajeruhi, kuwanyanyasa na kuwafukuza wananchi wa Ghaza. Kuanzia siku ya Ijumaa, idadi ya mashahidi imezidi kuongezeka na kufikia mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni wanawake, watoto na watu wasiokuwa na ulinzi. Jinai hii na uvamizi huu vinaendelea kufanyika huku ulimwengu ukiwa kimya, na mabeberu wa dunia wakiendelea kuwahami.
Maulamaa hao maarufu wa Bahrain wamemuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awarehemu ndugu zao waislamu wa Ghaza, wawashinde maadui zao, na awape msaada wa haraka.
Tamko hilo limetiwa saini na Ayatollah Sayyid Abdullah al-Ghuraifi, Sheikh Muhammad Sanqour, Sheikh Mahmoud al-‘Aali, na Sheikh Ali al-Sadadi
Maoni yako