Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, pombe inachukuliwa kuwa na hatari kubwa katika afya ya akili na nafsi, na inaweza kusababisha matatizo ya kisaikolojia pamoja na tabia za kikatili.
Swali:
Kwa nini Pombe imeharamishwa kwenye Uislamu?
Jawabu kwa muhtasari:
Mojawapo ya sababu kuu za kuharamishwa kwa Pombe katika uislamu ni kwamba Pombe inaharibu akili ya mwanadamu, takwimu zinaonesha kuwa walevi wa Pombe hupoteza akili zao taratibu na hatimaye kuwa wendawazimu, Pombe huondoa hadhi ya mwanadamu na kuishusha hadi kuwa sawa na mnyama.
Lakini madhara ya pombe hayaishii tu kwenye kupotea kwa akili. Pale ambapo mtu hana tena akili timamu, huwa tayari kufanya uovu wa aina yoyote, kutokana na kuzingatia madhara na athari zote mbaya za pombe, usilamu umeamua kuharamisha kabisa utumiaji wa kinywaji hiki hatari.
Maoni yako