Kwa mujibu wa idara ya kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, matembezi na hafla ya Siku ya kimataifa ya Quds yalifanyika katika mji mkuu wa Niger Niamey, kama ilivyokuwa katika mataifa mengine ya kiislamu, hafla hiyo ilihudhuriwa na balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wanazuoni wa kishia, wahubiri, wanafunzi, na waislamu waliokuwa wamefunga katika chuo kikuu cha Al-Mustafa.
Watu hao huku wakiwa kwenye mfungo walipaza sauti zao wakisisitiza mshikamano na umoja wao na Palestina dhidi ya wavamizi wa kizayuni na waungaji mkono wao madhalimu, huku wakidai ukombozi wa Quds Tukufu na ardhi ya Palestina.
Maoni yako