Jumatano 19 Machi 2025 - 06:17
Ni muda gani yatupasa kufanya Istikhara?

Ayatollah Jawadi Amuli amesema: Istikhara ni kuomba kheri, lakini ile istikhara ambayo mtu huifanya kabla ya kufikiria, kabla ya kushauriana, kabla ya kufanya tathmini, na kuamua moja kwa moja kuifanya kwa kutumia Qur’ani, hatukupewa maarisho ya kulifanya hilo.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka katika Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Jawad Amuli aliandika makala kuhusu mada ya "Istikhara" na alisema: Kufanya "Istikhara" kumegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni dua maalum ya istikhara, ambapo kwa kweli mwanzoni mwa dua hii hadi mwisho wake ni nuru, na hii ipo katika  kitabu cha "Sahifa Sajadiya".

Mtu yeyote anayepanga kufanya jambo, hata kama jambo lile linaonekana kuwa ni jema, anapaswa kuomba kheri kutoka kwa Mwenyezimungu kabla ya kulianza jambo lile, Hii ni amri ya Kiislamu na ni moja ya sunna zetu, na ni jambo zuri sana kulifanya.

Dua hii ya istikhara ni kuomba kheri, yaani: "Ewe Mwenyezimungu, mimi nimesha fikiria jambo hili, na dhahiri yake linaonekana kuwa na manufaa, lakini mimi siijui hatma yake, na wala siijui ni mambo gani yaliyo ambatana na jambo hili, tafadhali nakuomba uniwekee kheri katika jambo hili."

Istikhara ya aina hii maana yake ni kuomba kheri. Lakini ile istikhara ambayo mtu anaifanya kabla ya kufikiri, kabla ya kushauriana, kabla ya kufanya tathmini,  kwa haraka hufanya istikhara kwa kutumia Qur’ani, Istikhara ya aina hii hatujapokea maamrisho kwamba tuifanye.

Japokuwa wakati mtu anapokuwa amepatwa na shaka katika jambo fulani na hana hakika nalo, hapo anaweza kufanya Istikhara, lakini mwanzo tu wa jambo afanye Istikhara hivyo sio sahihi.

Kwa hivyo kuna mambo matatu muhimu:
1- Dua ya istikhara haipaswi kusahaulika.
2- Katika kila jambo, yatupasa kufikiri, kuzingatia, kushauriana, kutathmini, na kutumia akili.
3- Ikiwa mtu anakosa uamuzi (atakuwa kwenye shaka) hajui ni jambo lipi linalofaa na ni jambo lipi lisilo faa, basi wakati huo anaweza kufanya istikhara kwa kutumia Qur’ani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha