Jumanne 3 Novemba 2026 - 13:03
Jibu la dhati na la upendo la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, kwa barua ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi

Barua ya Alireza ilimfikia Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, akijibu upendo uliooneshwa na mwanafunzi huyo, alimwandikia barua na naye akampa zawadi kama ishara ya kumjibu kwa wema.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, siku chache zilizopita, Alireza Bakhshi Iraj, mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi anayeishi Tehran, aliandika barua ya dhati kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, tarehe 23 Shahrivar 1405.

Katika barua hiyo, pamoja na kueleza upendo wake na kutoa shukrani kwa mwongozo wa Kiongozi huyo, mwanafunzi huyo pia aliwasilisha zawadi kwa ajili yake, ikiwa ni ishara ya shukrani na mchango wa kuwasaidia wapiganaji wa Kiislamu.

Maudhui ya barua ya mwanafunzi huyo yalikuwa kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu

Salamu, Kiongozi wangu. Mimi ni Alireza Bakhshi, nina umri wa miaka kumi na ninaishi mjini Tehran.

Kwa kweli, sijui kama barua yangu itakufikia au la, natamani ingewezekana kuzungumza nawe ana kwa ana, kwa kweli tunalo deni kubwa kwako kutokana na mwongozo wako.

Fedha hizi pia ni kwa ajili ya kukushukuru na kuwasaidia wapiganaji wa Kiislamu, ninatamani kukutana nawe.

Alireza Bakhshi Iraj
23/6/1405

Tanbihi: Heri ya siku yako ya kuzaliwa, ingawa salamu hizi zimechelewa.

Barua hii ilimfikia Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, akijibu upendo uliooneshwa na mwanafunzi huyo, alimwandikia barua na naye akampa zawadi kama ishara ya kumjibu kwa wema.

Maudhui ya jibu la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.

Rafiki yangu mpendwa, Bwana Alireza Bakhshi,

Amani iwe juu yako, pamoja na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka Zake.

Ninakushukuru kwa namna yako ya upendo na kujali. Hata hivyo, siku ya kuzaliwa kwa mja huyu mnyenyekevu ni katika mwezi wa Esfand. Kwa upande wangu, nami ninakukabidhi zawadi, hata kama ni ndogo, kama malipo ya ukarimu wako.

Tafadhali fikisha salamu zangu kwa familia yako.

Sayyid Mojtaba Khamenei
19/Mehr/1405

Tanbihi: Una mwandiko mzuri na unaosomeka vizuri.

Jibu la dhati na la upendo la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, kwa barua ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi

Jibu la dhati na la upendo la Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu Iran, kwa barua ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha