Jumanne 22 Septemba 2026 - 10:32
Ayatullah Al-Udhma Shubairi Zanjani Kwa Hakika Alikuwa wa Kipekee Katika Elimu, Matendo na Uchamungu

Ayatullah Al-Udhma Nuri Hamadani ametoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia faqihi mashuhuri, Ayatullah Shubairi Zanjani.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ujumbe kamili wa rambirambi wa Ayatullah Al-Udhma Nuri Hamadani kufuatia kufariki dunia Ayatullah Shubairi Zanjani (ra) ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na hakika kwake Yeye tutarejea.

Habari ya kufariki dunia Marji' mwenye hadhi ya juu na faqihi wa Ahlul-Bayt watoharifu (amani iwe juu yao), Ayatullah Al-Udhma, Bwana Haj Sayyid Musa Shubairi Zanjani (ra), imeniletea huzuni na masikitiko makubwa.

Ninachokieleza kuhusu mwanazuoni huyu wa kimungu ninakisema kutokana na utambuzi wa kina nilioupata kupitia masomo tuliyoshirikiana mbele ya Ayatullah Al-Udhma Borujerdi na Muhaqqiq Damad (Mwenyezi Mungu awarehemu wote wawili), pamoja na tafiti na vikao vya kielimu tulivyoshiriki kwa miaka mingi.

Alikuwa mtu mwenye haiba na nafasi ya kipekee, aliyebobea katika elimu mbalimbali za fiqhi, Usul na Rijal, na kwa hakika katika zama zetu alikuwa wa kipekee katika elimu, matendo na uchamungu. Katika mambo yote alikuwa akimwona Mwenyezi Mungu pekee, na alikuwa mbali na dunia kwa maana halisi ya neno hilo. Alitumia maisha yake yenye baraka katika kueneza utamaduni wa Maasumina (amani iwe juu yao).

Vitabu vyake vyenye thamani pamoja na maneno yake adhimu yaliyokusanywa na mwanazuoni mheshimiwa Bwana Mukhtari, ni vyenye manufaa makubwa sana kwa wanazuoni wa dini, hawza imepoteza moja ya nguzo zake muhimu.

Mimi, kwa niaba yangu, natoa salamu zangu za rambirambi kufuatia kufariki dunia faqihi huyu mwenye hadhi ya juu, kwa Mtukufu Baqiyatullah Al-A’dham (Mwenyezi Mungu Aharakishe kudhihiri kwake), Hawza, watoto wake watukufu na wanazuoni, ndugu yake mpendwa, pamoja na Mashia wote na wapenzi wake. Namuomba Mwenyezi Mungu amjaslie daraja bora marehemu huyo mwema.

Qum: Hussein Nuri Hamadani

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha