Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Sami Abi al-Muna, Sheikh wa Aqli wa madhehebu ya Muwahhidin Druze, wakati akipokea ujumbe ulioundwa na masheikh na watu mashuhuri wenye ushawishi kutoka makabila ya Kiarabu katika maeneo ya Biqaa ya Kaskazini, Kati na Magharibi, pamoja na nchini Syria, katika makazi yake katika eneo la «Shaniyah», alisisitiza kuwa: Njia pekee ya kuliokoa taifa ni watu kuwa na umoja na kutafakari kwa kina kuhusu matokeo ya mambo, katika kukabiliana na uchokozi wa wazi ambao haujali kabisa maazimio ya kimataifa wala makubaliano. Aliongeza kuws: Ili kufikia utulivu, namna ya kukabiliana na uchokozi wa utawala wa Kizayuni inapaswa kuchunguzwa upya na kwa makini.
Aliendelea kusema: Amani na adui mnyakuzi, dhalimu anayefuata ndoto ya kutawala na kupanuka zaidi, haiwezekani. Hata hivyo, utulivu pia hautapatikana isipokuwa kwa kuondoka kikamilifu “Israel”, kurejea raia katika makazi yao, pamoja na serikali kubeba wajibu wake na kuwahakikishia watu usalama na maisha yao.
Abi al-Muna alisisitiza: Tunaunga mkono kila juhudi ya kuleta umoja wa neno na kuziba nyufa popote zilipo, iwe Lebanon au Syria. Hakuna silaha iliyo na nguvu zaidi dhidi ya miradi ya kujitenga na kueneza mifarakano kuliko silaha ya kushikamana na maadili haya, umoja wa msimamo na kuwa macho dhidi ya miradi ya uchochezi wa fitina inayosukwa na adui huku na kule.
Maoni yako