Jumamosi 14 Februari 2026 - 02:00
Taa za mapambo ya Ramadhani nchini Ubelgiji kwa mara ya kwanza katika historia

Hawza/ Manispaa ya mji wa Ghent nchini Belgium imetangaza kuwa, inakusudia kwa mara ya kwanza kufunga taa za mapambo ya mwezi wa Ramadhani katika vituo viwili maarufu vya ununuzi vya jiji hilo. Hii ni mara ya kwanza kwa mpango kama huo kufanyika kwa kiwango cha kitaifa nchini Ubelgiji.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, taa hizi za mapambo zitawekwa katika maeneo mawili yenye msongamano mkubwa wa watu katika mji huo wa Ubelgiji, ambayo yanajulikana kwa shughuli nyingi za kibiashara na uwepo wa idadi kubwa ya maduka yenye wauzaji Waislamu.

Kwa mujibu wa ripoti za Flanders News, takribani wafanyabiashara 100 wa rejareja wa eneo hilo wanaunga mkono mradi huu.

Waandalizi wa mradi huu wa kitamaduni wa Kiislamu wanasema kuwa juhudi hii inaakisi umuhimu wa mwezi wa Ramadhani kama kipindi muhimu cha kitamaduni na kidini kwa wakazi wengi wa Ubelgiji.

Mmoja wa wafanyabiashara wa Kiislamu katika mahojiano alisema: “Kwa miaka mingi tumekuwa tukiomba jambo hili, na tunafurahi kwamba hatimaye linatimia.”

Chanzo: About Islam

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha