Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Kashmiri, aliyekuwa arifu mashuhuri, alianza njia ya kuwalea wanafunzi wake kupitia hatua mbili za msingi: kuacha kabisa maharamisho na kutekeleza kwa makini wajibu wa kisheria.
Ayatullah Qaemi, mwanafunzi wake, anasema: “Kwa kawaida, ukamilifu unaowajia waja wa Mwenyezi Mungu hujitokeza baada ya hatua ya kuacha maharamisho na kufanya wajibu wa dini.”
Iwapo angeona kwamba mtu tayari amepita hatua hiyo, si mtu wa kufanya madhambi, na wala haachi hata wajibu mmoja, basi alikuwa akisema mambo mengine zaidi; mfano, anamuhusia mtu amuelekee Mungu zaidi, au angempa adhkari fulani, hapo ndipo alikuwa akianza.
Chanzo: Kitabu Sheydā, uk. 88
Maoni yako