Jumapili 23 Novemba 2025 - 23:25
Uswisi Yawa Mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Nafasi ya Misikiti

Hawza/ Uswisi imekuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa kuchunguza nafasi ya misikiti na mchango wake unaozidi kuongezeka katika maendeleo ya kijamii ya jamii za Ulaya.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika mkutano huu, wazungumzaji walisisitiza kuwa ushiriki hai wa misikiti barani Ulaya ni miongoni mwa malengo ya mipango ya kielimu, na mojawapo ya mikakati ya mazungumzo ya dini pamoja na shughuli za kiutu.

Kwa hakika, jambo hili ni miongoni mwa nyenzo zenye ufanisi mkubwa katika kupunguza mvutano wa kitamaduni na kuimarisha uelewa wa wazi wa Uislamu wa kweli na Waislamu, na linaweza kuwa chombo chanya na chenye kujenga katika jamii za Magharibi.

Vilevile, viongozi wa Albania waliokuwepo katika mkutano huu walitoa taarifa kuhusu maendeleo ya nchi yao katika uwanja wa ukuaji na ustawi wa misikiti ya Albania, na wakabainisha mipango yao kwa ajili ya nchi nyingine za Ulaya.

Chanzo: Aljazeera

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha