Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Mu’in al-Kāzimī, mmoja wa viongozi wa Muungano wa Uratibu nchini Iraq, katika mahojiano na kipindi cha “Alanan” kinachorushwa na kituo cha Al-Sumariyya, alisisitiza kwamba kipindi cha pili cha uwaziri mkuu wa Muhammad Shiyā‘ al-Sudānī kinawezekana, kwa sharti kwamba atoe dhamana kuhusu mtindo wake wa uongozi kwa hatua ijayo.
Al-Kāzimī alisema: Muungano wa Uratibu haujumuishi upande wowote mkali au wenye misimamo ya kupendelea upande mmoja unaotafuta kuhodhi uwakilishi wa Waislamu wa Kishia, na akasisitiza kwamba kazi ndani ya Muungano huu inajengeka juu ya maelewano na ushirikiano kati ya vipengele vyake vyote.
Akaongeza: Kuongezewa muhula wa pili wa uwaziri mkuu wa Muhammad Shiyā‘ al-Sudānī bado ni chaguo linalowezekana, kwa sharti kwamba atoe dhamana kuhusu mtindo wake wa uongozi kwa hatua ijayo na kuwa katika mwafaka na mtazamo wa Muungano wa Uratibu.
Al-Kāzimī alibainisha kuwa; ombi la moja ya pande za Kisunni kudai nafasi ya urais ni propaganda ya kisiasa tu, na akasisitiza kuwa kauli hiyo haiakisi maelewano ya sasa ya nguvu za kisiasa.
Maoni yako