Jumapili 9 Novemba 2025 - 11:06
Janga la Sudan na Nafasi ya Israel katika Mauaji ya Wanawake na Watoto

Hawza/ Sudan imejikuta ikikabiliwa na vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe; mapigano kati ya jeshi la serikali linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) linaloongozwa na Muhammad Hamdan Dagalo, anayejulikana kwa jina la “Hemedti.” Kuanguka kwa mji wa Al-Fashir na mauaji ya halaiki ya raia kumeonesha kuwa mgogoro huu si mzozo wa ndani pekee, bali umefungamana moja kwa moja na kuingilia kati kwa Israel na baadhi ya nchi nyingine.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Tangia mwaka 2023, Sudan imekuwa uwanja wa vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe; vita kati ya jeshi linaloongozwa na al-Burhan na Jeshi la Msaada wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Hemedti. Mzozo huu wa ndani, kutokana na kuhusika kwa wachezaji wa kigeni, umegeuka kuwa suala lenye sura za kisiasa za kikanda.

Nafasi ya Israel pia ni ya msingi na yenye kuleta machafuko. Tel Aviv ilikuwa na uhusiano na pande zote mbili — al-Burhan na Hemedti — lakini katika miezi ya karibuni imeonekana wazi kumuunga mkono kiongozi wa RSF. Israel imewapa waasi hao teknolojia za hali ya juu za ujasusi.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha