Jumatano 20 Agosti 2025 - 21:00
Kuitambua Rasmi Palestina; Udanganyifu Mpya wa Magharibi na Wazayuni

Hawza/ Kuitambua dola ya Palestina na baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu, si zaidi ya msaada wa kweli, bali ni maonesho ya kisiasa kwa ajili ya kupunguza shinikizo la mitazamo ya umma na kuthibitisha kuenea kwa utawala wa Kizayuni, Wataalamu mashuhuri wanaamini kuwa hatua hii bila ya shinikizo la kweli dhidi ya Israel, haitakuwa chochote isipokuwa hila ya kudhoofisha mapambano na kulinda hali iliyopo

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, utawala wa Kizayuni ukiwa na tegemeo la ujanja na nguvu za kijeshi, daima umefanya jitihada za kuendeleza ukaliaji wa mabavu na kuwakandamiza Wapalestina, kuitambua Palestina bila shinikizo la kweli, kwa hakika ni chombo cha kufunika ukweli huu na udanganyifu wa fikra za umma na Magharibi pamoja na Israel.

Utangulizi

Kuitambua dola la Palestina kutoka kwa nchi za Magharibi si alama ya msaada wa kweli, bali ni chombo cha kuuzalisha tena utawala huo katika sura mpya, kwa kutegemea tajiriba za kihistoria na uelewa wa mienendo ya nguvu za kikoloni, hatua hii inachukuliwa kama jaribio la kuitengeneza Palestina isiyo na hatari, isiyo na mapambano na hatimaye kuthibitisha utawala wa Kizayuni.

Maamuzi kama haya, badala ya kutoka kwenye mshikamano wa kweli na taifa la Palestina, ni mbinu za kisiasa kwa ajili ya kusimamia uwanja wa kisiasa na kimaeneo ya habari, wakati ambapo Ghaza ipo chini ya mashambulizi ya mabomu na vizuizi vikali, mgogoro wa kibinadamu umefikia kileleni na mapambano ya Palestina yamepata uhalali usio na mfano katika fikra za watu duniani, wakati huohuo, utawala wa Kizayuni umehukumiwa katika vyombo vingi vya habari vya Magharibi kuwa unafanya mauaji ya kimbari huku wimbi la ghadhabu na mshikamano na watu wa Palestina likiibuka.

Katika mazingira haya, kutumia misemo kama “amani”, “mataifa mawili” na “ujenzi upya wa Ghaza” kimsingi kumekuwa chombo cha kupunguza shinikizo la fikra za umma na kupotosha jinai zinazofanywa na Israel.

Kuitambua Palestina; Maonesho kwa ajili ya kutuliza fikra za umma

Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya nchi za Magharibi na Kiarabu zimethubutu kutangaza kuitambua dola ya Palestina, lakini jambo la msingi kufahamu ni kuwa; hatua hii si kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Palestina, bali ni zaidi ya maonesho ya kisiasa na yenye fitna kwa ajili ya kuzihadaa fikra za umma.

Nchi hizi kwa kitendo hiki zinataka kuwaonyesha wananchi wao kwamba “wamefanya jambo fulani”, na kwa kupunguza shinikizo la mitazamo ya umma, kuzima maandamano makubwa; hali ambayo kivitendo hakuna mabadiliko yoyote yanayotokea Palestina na ukaliaji wa mabavu pamoja na dhulma unaendelea.

Aina hii ya kuitambua, inawasilisha picha ya Palestina dhaifu na tegemezi ambayo haina mamlaka ya kusimamia ardhi yake, haina nguvu ya kijeshi ya kujitegemea, na haina uwezo wa kweli wa kutetea haki za wananchi wake, kwa hakika, Palestina ambayo Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu wanataka kuitambua, ni dola iliyo kwenye karatasi tu, ambayo kwa vitendo ni chombo cha maslahi yao na haiwezi kutambua mapambano halali ya watu wa Palestina.

Huu ni mtego wa kisiasa ambapo mipaka na rasilimali hubaki mikononi mwa Israel, Palestina hubaki imegawanyika katika maeneo machache yaliyohusuriwa, na hata mapambano ya kiraia kwa mujibu wa makubaliano hugeuzwa kuwa kosa na kuitwa “ugaidi”. Hatimaye, fikra za umma duniani zitahisi kwamba “tatizo la Palestina limesha tatuliwa” na shinikizo dhidi ya Israel hupungua.

Tajiriba chungu ya zamani; kurudiwa kwa hadithi ile ile

Tajiriba ya makubaliano ya Oslo mnamo mwaka 1993, ambayo yalikuwa makubaliano ya upande mmoja kwa faida ya wakaliaji mabavu wa Kizayuni na kutiwa saini na Yasser Arafat na Yitzhak Rabin, ilionesha kuwa mienendo kama hii imesababisha kudhoofisha mapambano ya Wapalestina na kuendelea ukaliaji wa mabavu, Kwa dhahiri, yalitarajiwa makubaliano hayo yangepelekea kuundwa kwa dola ya Palestina, lakini ujenzi wa makazi ya Kizayuni haukusimama, bali uliongezeka maradufu.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina ikageuka kuwa mkono wa kiusalama wa Israel na ukaliaji wa mabavu ukaendelea kwa sura “halali”.

Makubaliano ya Oslo yaliipa Israel muda wa kudhoofisha mapambano ya Wapalestina na wakati huo huo kujipatia uhalali wa kimataifa ili kuendeleza ukaliaji wa mabavu kwa dhahiri, Wapalestina walipata madaraka, lakini kivitendo udhibiti wote uliendelea kubaki mikononi mwa Israel.

Leo pia hadithi ile ile inarudiwa; kuwapa Wapalestina dola kwa jina bila ya kumaliza ukaliaji wa mabavu na bila kuwapatia haki za kimsingi za watu wa Palestina, hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kumwamini mbwa mwitu ambaye ameshambulia mara kadhaa, nchi za Magharibi na Kiarabu pia zinaufahamu mchezo huu, na badala ya kutafuta haki, malengo yao ni kuzima maandamano ya ndani na kupunguza shinikizo la mitazamo ya umma wao.

Kwa nini Marekani na utawala wa Kizayuni wanapinga kwa sura ya nje?

Kwanza: Wanataka mchakato huu uonekane kama “fursa” ambayo inapaswa kutolewa katika majadiliano na kwa masharti ya Israel kwa Wapalestina.

Pili: Wanataka kuonesha fikra za umma (hasa ndani ya Israel na Marekani) kwamba “hatusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa” ili kulinda nafasi zao za kisiasa ndani.

Tatu: Kwa kupinga kwa sura ya nje, wanapandikiza wazo kwamba kuundwa kwa dola ya Palestina lazima kuwe kwa masharti ya Israel: kuondoshwa kabisa silaha za makundi ya mapambano, kufutwa kwa Hamas na Jihad al-Islami kutoka kwenye siasa, kuitambua Israel kama “dola ya Kiyahudi”, na kuachia udhibiti wa mipaka, anga na rasilimali kwa Israel.

Kwa njia hii, iwapo siku moja dola hii “litatengenezwa”, wote watasema: “Tazama! Hata Israel imekubali”; hali ambayo kimsingi litakuwa ni dola ile ile ambayo tangia mwanzo Israel na Marekani wameipanga.

Matokeo ya mwisho; kuangamizwa kwa Palestina halisi

Kwa hakika, aina hii ya kuitambua Palestina ni mfano wa kifuniko kisichobadilisha hali ya Palestina, bali ni tiba ya muda ya ghadhabu za watu, Kama Magharibi kweli ingeiruhusu Palestina, ingelazimisha shinikizo la kweli dhidi ya Israel; kama vikwazo au vitisho vya kidiplomasia, lakini jambo hili halitokei, na badala yake ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi na Israel unaendelea.

Kwa hivyo, Palestina inayotambuliwa katika taasisi za kimataifa si Palestina halisi, bali ni chombo cha kuhifadhi maslahi ya Magharibi na Israel na kukandamiza mapambano ya kweli.

Kwa sentensi moja: Utambuzi huu si hatua kuelekea ukombozi wa Palestina, bali ni hatua ya mwisho ya kuifunga ndani ya gereza la kidiplomasia; gereza ambalo kufuli lake limetengenezwa na Israel na ufunguo wake upo mikononi mwa Washington.

Mitazamo ya baadhi ya wataalamu kuhusu kuitambua Palestina

Ilan Pappé: Mwanahistoria na mwandishi Muisraeli mpinga-Uzayuni, ambaye katika vitabu vyake kama “Ethnic Cleansing of Palestine” ameonesha kwa mapana jinsi mikataba na makubaliano ya juu juu vimekuwa kisingizio cha kuendeleza ukaliaji wa mabavu, anaamini kuitambua dola ya Palestina bila shinikizo la kweli dhidi ya Israel ni bure na ni udanganyifu.

Yousef Munayyer: Mchambuzi Mpalestina-Mmarekani ambaye katika tovuti ya Middle East Eye na vyombo vingine ameandika wazi, kwa nini nchi nyingi zinaitambua Palestina kwa shinikizo la mitazamo ya umma tu bila kuchukua hatua za kivitendo dhidi ya Israel.

Abdul Bari Atwan, mchambuzi maarufu wa Kiarabu: Kuitambua Palestina na baadhi ya nchi ni mchezo na udanganyifu ulioundwa ili kuiokoa taswira ya Israel kutoka kwenye chuki ya umma.

Hujjat al-Islam Sayyid Jawad Naqvi, miongoni mwa wanazuoni mashuhuri: Kuitambua dola ya Palestina kwa hakika si msaada kwa Wapalestina bali ni hila ya kuthibitisha uhalali wa Israel.

Azmi Bishara, mwanazuoni wa Kipalestina na mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Kiarabu cha Siasa: Anaona kuwa utambuzi huu ni “kukubali Palestina kama alama, si kama uhalisia wa kisiasa”, na bila haki ya kurejea, bila kumaliza ukaliaji wa mabavu na bila mapambano, ni dola ya kufikirika tu.

David Miller, profesa wa sosholojia ya siasa na mkosoaji wa lobi ya Kizayuni: Kwa mtazamo wake, mchakato huu ni sehemu ya hila kubwa zaidi kwa ajili ya kusonga mbele mradi wa Kizayuni katika ukanda hui, na lengo lake ni kuidhibiti kabisa harakati ya muqawama na kuupanua ushawishi wa Israel.

Ramzy Baroud, mwandishi wa habari na mwandishi Mpalestina: Anaamini kuwa kuitambua bila shinikizo la kweli dhidi ya Israel ni “kubadilisha vifungashio” vya suala la Palestina na hakumalizi ukaliaji wa mabavu

Naqi Amini

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha