Alhamisi 30 Aprili 2026 - 01:30
Vita vya leo ni makabiliano ya pande zote za Uislamu dhidi ya kambi ya ukafiri/ Iran ni mstari wa mbele katika muqawama wa Kiislamu

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hussein Hadi, mkurugenzi wa Taasisi ya Mtume Mtukufu (s.a.ww) mjini Kabul, katika warsha ya mtandaoni “Imam Khamenei; Kiongozi Shahidi” iliyofanyika Jumanne kwa juhudi za Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu, huku akisisitiza kwamba; vita vinavyoendelea haviko tu ndani ya Iran, alivieleza kuwa; ni makabiliano ya pande zote ya Uislamu dhidi ya kambi ya ukafiri, na akasisitiza umuhimu wa Waislamu wote kuiunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mhimili wa muqawama.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Hussein Hadi, mkurugenzi wa Taasisi ya Mtume Mtukufu (s.a.ww) mjini Kabul, akiashiria kuuawa kishahidi Ayatullah Khamenei, alilitaja tukio hili kuwa limeleta heshima, kuinuka na kuimarika kwa umoja miongoni mwa Waislamu, na hata kuamsha dhamiri za kimataifa, akasema: Tukio hili halikuishia ndani ya nchi za Kiislamu pekee, bali pia katika kiwango cha kimataifa lilisababisha wimbi la mshikamano na mwamko.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mtume (s.a.ww) Kabul, pia alishukuru juhudi za Jumuiya ya Kimataifa ya Kukurubisha Madhehebu za Kiislamu na uongozi wake katika kuimarisha umoja wa Kiislamu, na akaongeza: Katika hali ambayo baadhi ya mikondo inachochea mgawanyiko, taasisi hii inaendelea katika njia ya kukurubisha madhehebu, udugu na mwamko wa Kiislamu.

Aliendelea kwa kukosoa mitazamo inayoviona vita vya hivi karibuni kama mzozo tu kati ya Iran na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni, na akasisitiza: Uchambuzi kama huo ni wa juu juu na wenye mipaka; kwa sababu iwapo maadui wangefanikiwa kuidhoofisha au kuigawa Iran, miradi mikubwa zaidi ya kugawa na kudhoofisha nchi nyingine za Kiislamu ingeendelea katika mfumo wa mipango kama “Mashariki ya Kati Mpya.”

Hujjatul-Islam Hadi, huku akisisitiza nafasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mstari wa mbele wa kambi ya Uislamu, alisema: Watu wa Iran na mhimili wa muqawama kwa kusimama imara, kujitoa mhanga na kutafuta shahada wameonesha kwamba wako katika njia ya kutetea maslahi ya umma wa Kiislamu, na kwamba vita hivi kwa hakika ni makabiliano ya “Uislamu wote dhidi ya ukafiri wote.”

Alisema kuwa kuiunga mkono Iran na mhimili wa muqawama kuwa ni wajibu wa pamoja, na akaongeza: Waislamu wote wanapaswa kwa kila njia waliyonayo kuchukua hatua katika njia ya mshikamano, ushirikiano na kusimama pamoja na taifa la Iran na mhimili wa muqawama.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake huku akirejea malengo ya maadui ya kuleta machafuko na kutawala eneo hilo, alisema: Baadhi walidhani kwamba mashambulizi haya yangepelekea kugawanyika kwa Iran na kuimarika kwa nafasi ya watu kama Benjamin Netanyahu, lakini kuuawa kishahidi kwa kiongozi wa mapinduzi hakukufanikisha malengo hayo, bali kulisababisha mshikamano mkubwa zaidi ndani ya taifa la Iran, nchi za Kiislamu na hata maoni ya umma duniani.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha