Ijumaa 20 Machi 2026 - 15:10
Ofisi ya Ayatollah Sayyid al-Sistani: Jumamosi ndio Siku ya Kwanza ya Mwezi Shawal na Sikukuu ya Eid al-Fitr

Hwaza/ Ofisi ya Marji' Mkuu Ayatollah Sayyid al-Sistani mjini Najaf, Iraq, imetangaza kupitia tamko rasmi kuwa; Jumamosi itakuwa ni siku ya kwanza ya Mwezi Shawal na Sikukuu ya Eid al-Fitr kwa mwaka 1447 wa Hijria Qamaria, (2026).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ofisi ya Ayatollah Sayyid al-Sistani imesema kuwa; Ijumaa itakuwa ni mwisho wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani (siku ya 30) na Jumamosi, tarehe 21 Machi 2026 (1 Farvardin 1405 H.S), itakuwa ni siku ya kwanza ya Mwezi Shawal na Eid al-Fitr.

Aidha, Kamati ya Kutangaza Mwezi (Estihlal) ya Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia imetangaza kwamba; Jumamosi itakuwa ni siku ya kuuanza Mwezi wa Shawal. Kamati hiyo imesema kuwa; hakukuwa na uthibitisho wa kuonekanwa mwezi usiku wa Alhamisi, tarehe 29 ya Ramadhani, na kwa hiyo Mwezi huu wa Ramadhani utakuwa na siku 30, na siku ya Jumamosi itakuwa ni siku ya kwanza ya Shawal na Eid al-Fitr.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha