Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa habari wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Sayyid Muhammad Saidi katika khutba za Swala ya Ijumaa tarehe 4 Mehr 1404 katika Musalla Quds Qom Iran, akirejelea maelekezo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisema: Marekani katika uso wa mbele, Wazayuni nyuma ya pazia, na Ulaya katikati ya uwanja, kwa“Kwa visingizio mbalimbali waliendeleza hatua ya kuamsha utaratibu wa kurejesha vikwazo na wakaweka mstari wa ubatili juu ya mikataba yote".
Akaendelea kusema: Marekani na Trump muovu na mjeuri pamoja na washirika wake kwa maneno ya mara kwa mara ya jeuri na matarajio ya ubeberu baada ya shambulio la moja kwa moja dhidi ya vituo vya nyuklia, waligeukia kuwatishia Wairani na kudai kwa ujeuri mkubwa kusitishwa kikamilifu kwa urutubishaji wa nyuklia, na wakati huo huo waliweka vikwazo. Walidhani kwamba kwa mbinu hizi, hatua za Iran zitazorota na taifa litakubali mazungumzo ya udhalilishaji.
Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qom, akirejelea safari ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu kwenda New York, alisema: Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, kama mwakilishi wa taifa kubwa la Iran, baada ya vita vya kulazimishwa vya siku kumi na mbili, alielekea New York ili kwa mujibu wa maneno ya Amirul-Mu’minin (a.s.) anayesema:
«کونوا لِلظّالِمِ خَصمًا وَلِلمَظلُومِ عَونًا»“Kuwa adui wa dhalimu na msaidizi wa aliye dhulumiwa”
Kufikisha sauti ya taifa la Iran lililo madhulumu na lenye nguvu, akiwa ameambatana na picha za mashahidi waliouawa kwa dhulma mikononi mwao, na vilevile kufikisha sauti ya watu wanyonge wa Ghaza masikioni mwa walimwengu.
Akaongeza: Baadhi ya waliovutiwa na Magharibi na wenye kuuza taifa walipendekeza kukutana kwa Rais wa Iran na muuaji wa watu wasio na hatia wa nchi yetu, katika mazingira haya, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisimama imara na kwa upinzani wa wazi kabisa alieleza kuwa mazungumzo katika hali kama hii ni hasara tupu, na upande mwingine akabainisha waziwazi upinzani wake dhidi ya utengenezaji wa silaha za nyuklia, akifafanua kwamba mpango wa nyuklia ni wa matumizi ya amani pekee.
Imamu wa Ijumaa wa Qom alisema: Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi alisisitiza kuwa lazima itoke sauti moja kutoka Iran ili mkono wa mwakilishi wa wananchi wa Iran katika mazungumzo uwe na nguvu, na aweze kusimama imara mbele ya ujeuri wa Wamagharibi. Wanasiasa wanapaswa kuonyesha ramani ya njia na mwelekeo wa baadaye. Aliwakumbusha wote kwamba jitihada za kuifanikisha “Iran yenye nguvu” ndio njia pekee ya kutatua matatizo ya wananchi na nchi.
Msimamizi wa Haram ya Bibi Ma‘suma (a.s.) alieleza: Kwa kufanikisha mkakati huu, yaani “Iran yenye nguvu”, waliifahamisha dunia kwamba makadirio yao juu ya kulegea kwa Iran si chochote bali ni dhana tupu, na taifa la Iran litapiga ngumi thabiti kwenye midomo ya waropokaji.
Akaeleza kuwa: Qur’ani Tukufu inayatambulisha maisha yenye mwenendo mwema na wa kimungu kwa jina la “حياة طيبة” (maisha safi) na katika aya ya 97 ya Suratu Nahl inasema:
«مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِنْ ذَکَرٍ أَوْ أُنْثَیٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْیِیَنَّهُ حَیَاةً طَیِّبَةً»“Atakayefanya mema, awe mwanaume au mwanamke, naye ni muumini, basi kwa yakini tutamhuisha maisha safi yenye baraka.”
Mwakilishi wa Waliyyul-Faqih Qom akaongeza: Kupata aina hii ya maisha kunategemea kushikamana na misingi yake.
Moja ya nguzo kuu za hayaatun ṭayyibah ni heshima ya kujistahi na haya katika mahusiano ya kijamii na kibinafsi, ikiwa uhusiano baina ya watu, hasa baina ya wanawake na wanaume, hautajengwa juu ya kanuni za haya na kujistahi, jamii itaelekea kwenye upotovu na kuvunjika kwa msingi wa familia.
Akasema kuwa: Katika hali kama hiyo, japokuwa wahanga wa moja kwa moja ni wanawake na mabinti, lakini jamii nzima itateseka kwa kuvunjika kwa msingi wa familia, mfarakano wa utambulisho, na uharibifu wa kimaadili, hivyo basi, kulinda usalama wa kijamii ni jukumu la kila mmoja.
Ayatollah Saidi katika khutba ya kwanza alisema: Imam Ali (a.s.) katika barua ya 53 ya Nahjul-Balagha baada ya kumhimiza Malik al-Ashtar juu ya taqwa, kuhusu matokeo ya taqwa anasema:
«أَنْ یَنْصُرَ اللَّهَ سُبْحَانَهُ بِقَلْبِهِ وَیَدِهِ وَلِسَانِهِ»“Yaani kila muumini mwenye taqwa kila wakati atakapoona dini ya Mwenyezi Mungu na malengo ya kimungu yanahitaji msaada wake, basi atamnusuru Mwenyezi Mungu kwa moyo wake, kwa mkono wake, na kwa ulimi wake.”
Khatibu wa Ijumaa wa Qom akasema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 129 ya Suratu Tawbah anamfariji Mtume (s.a.w.w) kwamba asivunjike moyo kwa ukaidi wa watu, na anasema:
«فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِیَ اللَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَیْهِ تَوَکَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِیمِ»“Basi wakigeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye tu. Mimi namtegemea Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi.”
Akaeleza kwamba aya hii ina nguzo tatu: Mwenyezi Mungu anasema: «حَسْبِیَ اللَّهُ» yaani muendeshaji wa mfumo wa uumbaji ni Mwenyezi Mungu na Yeye peke yake hutosheleza, hapana haja ya mwingine, «لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ» yaani utoshelevu ni miongoni mwa sifa za kiungu, na kwa kuwa uungu ni wa Mwenyezi Mungu pekee, basi utoshelevu pia ni wa Mwenyezi Mungu pekee.
Msimamizi wa Haram ya Bibi Ma‘suma (a.s.), akirejelea aya isemayo:
«عَلَیْهِ تَوَکَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِیمِ»,
Alisema: Mtu anapokuwa na imani
ya dhati na kushikamana kivitendo na misingi hii miwili ya imani, basi hutegemea na kutegemeza mambo yake yote kwa Mwenyezi Mungu Mmoja tu.
Akaeleza kuwa: Tawakkul maana yake ni kuyakabidhi na kuyaweka mambo yote mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Hasa katika suala la risala, ambalo ni jukumu kubwa na lenye changamoto, na zaidi katika uongozi na wilaya kwa jamii, changamoto ni nyingi mno. Ndio maana Mwenyezi Mungu katika aya ya 67 ya Suratu al-Māidah anasema:
«یَا أَیُّهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَیْکَ مِنْ رَبِّکَ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ وَاللَّهُ یَعْصِمُکَ مِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ لَا یَهْدِی الْقَوْمَ الْکَافِرِینَ»“Ewe Mtume! Fikisha yaliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako [kuhusu wilaya na uongozi wa Ali ibn Abi Talib (a.s.)]. Na kama hufanyi, basi hujafikisha risala ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu, hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri.”
Khatibu wa Sala ya Ijumaa ya Qom akaongeza: Aya hii inaonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w) alikuwa akikabiliana na wale waliokataa suala la wilaya na uongozi baada yake, na akawaambia kwa uwazi kuwa mimi sina hofu yoyote kutokana na nyinyi kukataa haki. Watu hawa aidha hawakuelewa hakika ya risala ya Mtume (s.a.w.w) au hawakutaka kuelewa, kwamba risala ya Mtume ilikuwa kwa ajili ya kuwaokoa kutokana na mateso na misiba.
Akasema kuwa: Upole, rehema na huruma ya Mtume (s.a.w.w) haukuwa msingi wa hisia za kikabila au kitaifa, bali yeye alikuwa chini ya amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa hiyo, hata kama watu wote wangegeuka, isimngemrudisha nyuma kutoka njia aliyochukua.
Imamu wa Ijumaa wa Qom akabainisha: Ujumbe wa aya hii unahusu zama hizi pia; yaani, ikiwa leo hii pia watu, tawala au harakati fulani hazitainama mbele ya misimamo ya haki ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na nyinyi taifa shujaa la Iran, basi msihofu wala msivunjike moyo, bali tangazeni kwa uwazi kuwa tegemeo letu liko kwa Mwenyezi Mungu.
Mwisho wa ujumbe
Maoni yako