Jumapili 2 Novemba 2025 - 15:32
Mpaka mwisho wa uhai tutailinda Palestina / Tuko tayari kwa aina yoyote ya mapigano

Hawza/ Mandhari za uwanja katika mikoa ya Amran, Rima, Hajjah, Ma’rib, al-Mahwit, Ta‘iz na al-Bayda zinaonesha kuendelea kwa harakati za umma za Yemen, zinadhihirisha uaminifu kwa mashahidi na zinasababisha kuongezeka kwa kiwango cha utayari wa kukabiliana na mpango wowote wa uvamizi bila kuyumba, huku zikitangaza msaada endelevu kwa watu wa Palestina na wapiganaji mashujaa wao.

Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, jana kulifanyika maandamano makubwa katika maeneo mbalimbali ya Yemen yaliyoandaliwa na vikundi vya basiji vya umma na makundi ya makabila - wenye silaha na wasio na silaha - ambapo watu wa Yemen, licha ya kusitishwa vita kuliko dhaifu huko Ghaza, walisisitiza kuwa iwapo mashambulizi ya Israeli dhidi ya watu wa Ghaza yataendelea, wako tayari kupigana dhidi ya uvamizi wa utawala wa Kizayuni.

Mtandao wa Al-Masirah uliandika kuhusu maandamano ya watu wa Yemen: Mandhari ya basiji wa umma na maandamano ya Ijumaa yameenea kote nchini na viwanja vimegeuka kuwa zaidi ya mabango ya muungano, uaminifu kwa mashahidi na tamko la utayari kamili wa kukabiliana na mpango wowote unaolenga umma wa kiislamu.

Mikoa mbalimbali ya Yemen yameshuhudia maandamano makubwa na mikutano ya makabila ambayo ilionesha ari ya kujitolea kitaifa na kidini na kuonesha uaminifu na msaada kwa taifa la Palestina na wapiganaji wa muqawama wao. Harakati hii ya umma ilibainisha utayari wa kukabiliana na tishio lolote, ilidhihirisha uvumilivu wa taifa la Yemen na nia yao isiyotetemeka ya kufuata njia ya mashahidi, na kuonesha ujasusi wa umma unaoendelea katika maeneo yote yaliyoachiliwa huru ya Yemen.

Katika mkoa wa Amran, wakazi wa wilayani na vijijini walifanya maandamano makubwa na mikutano ya kikabila, wakiwa wamebeba picha za mashahidi na wakionesha alama za mapambano, huku wakidhihirisha dhamira yao ya kuitetea dini na kuwaunga mkono walionyang’anywa haki.

Ujumbe ulilenga kuimarisha ushiriki katika programu za basiji kwa umma na kusisitiza utayari wa makabila kutekeleza maagizo ya sayyid Abd al-Malik Badruddin al-Houthi, kiongozi wa mapinduzi, na walituma ujumbe wazi kwa wadukuzi wote kwamba jibu kwa uvamizi wiwote litakuwa ni kali.

Katika mkoa wa Rima, washiriki  maandamano na mikutano walielezea uaminifu wao kwa roho ya jihadi na muqawama na uaminifu wao kwa mashahidi wakuu, na kusisitiza ahadi yao ya kuinua kiwango cha mafunzo na uwezeshaji na kuongeza utayari wa kukabiliana na njama yoyote itakayolenga taifa na wananchi.

Washiriki walisisitiza umoja wa safu za Wayeameni na utayari wao wa kutoa msaada wa dhati kwa taifa la Palestina endapo kutatokea uvamizi wowote wa Kizayuni.

Katika mkoa wa Hajjah, maandamano yenye silaha yalifanyika pia, ambapo washiriki walisisitiza dhamira yao ya kuhifadhi misingi ya kidini na ya kibinadamu na kutetea uhuru na rasilimali za nchi.

Washiriki waliwaonya wadanganyifu wote kuwa Yemen itabaki imara dhidi ya kila jitihada za kuleta machafukk ndani ya mipaka na wakabainisha kwamba basiji na juhudi za mafunzo ya kijeshi vitaendelea maradufu.

Kuhusu Ma’rib ya kihistoria, mji huo ulishudia mikutano ya umma na mikutano ya kikabila ambapo washiriki walionesha alama za uaminifu kwa mashahidi na kurudia kiapo chao cha kuiendeleza njia yao, na kusisitiza utayari wa watu huru wa Ma’rib kushiriki katika hatua yeyote inayofuata ya kupigana na adui wa Kizayuni. Walisisitiza kuimarisha basiji wa kijeshi na programu za mafunzo, na wakabainisha kwamba Ma’rib itaendelea kuwa ngome imara dhidi ya tishio lolote na basiji wa umma wataendelea bila kupingwa.

Katika mkoa wa al-Mahwit, wanaume huru walipanga maandamano makubwa yakiwa na ushiriki wa wanazuoni na watoto, ambapo walielezea fahari yao ya kuhifadhi imani na maadili mema.

Waliwatangaza basiji ili kuimarisha safu za nguvu za ulinzi na kuwapa vifaa pamoja na wapiganaji wenye sifa.

Katika mkoa wa Ta‘iz, baada ya Swala ya Ijumaa, maandamano yalifanyika katika maeneo mbalimbali na washiriki wakitoa shukrani kwa jitihada za muqawama wa Palestina hukk Ghaza, na kusisitiza kuwa bssiji na ushiriki wa jamii ndio njia ya kukabiliana na vitendo vyovyote vya uvamizi.

Walisisitiza utayari wao wa kupigana baharini na kumzuia adui wa Kizayuni, na wakibainisha eneo la Bab al-Mandab litabakia ni lenye kufungwa dhidi ya adui muda wa kuwa Ghaza ipo kwenye vizuizi, na kusisitiza kwamba uvamizi wowote utakaofanywa na taifa hilo, wa Yemen watatoa majibu.

Katika mkoa wa al-Bayda, mikusanyiko mikubwa ilifanyika katika maeneo mbalimbali ambapo washiriki waliweka wazi dhamira yao kamili ya kuifuata njia ya jihadi na shahada na walienda kuapa tena kwa mashahidi kwa ajili ya taifa, katika mstari wa mbele wakiwemo shahidi mpiganaji Muhammad Abd al-Karim al-Ghamari, na kusisitiza kuwa damu za mashahidi zitabakia kuwa taa ya njia ya uvumilivu na uaminifu, na kwamba basiji na mafunzo ya kijeshi vitaendelea bila kukoma.

Kwa muktadha huo, taarifa zilizotolewa za maandamano na mikusanyiko mbalimbali katika mikoa ya Yemen zilisisitiza kuendelea kwa basini na utayari kamili wa kukabiliana na mpango wowote wa uvamizi unaolenga taifa na wananchi, na kwa wakati mmoja walirudia kiapo chao cha kusimama imara katika njia ya mashahidi wakuu, hasa shahidi mpiganaji Muhammad Abd al-Karim al-Ghamari.

Takwimu hizi zinaonesha kwamba taifa la Yemen, pamoja na watoto wake na makabila yake, litabakia imara wanapokutana na kuongezeka kwa mzozo wowote, na litapinga kwa nguvu jitihada zote za kuleta hali ya sintofahamu au ukiukaji wa uhuru wa taifa, na kusisitiza msaada wao kwa vikosi vya ulinzi na vyombo vya usalama katika kuhifadhi usalama na utulivu.

Taarifa hizi pia zilikuwa na ujumbe wa wazi kwa jumuiya ya kimataifa na mashirika ya haki za binadamu, zikisema kuwa wana wajibu kwa ukimya wao kuhusu uvamizi wa Kizayuni na Marekani, na walitaka msaada kwa taifa la Palestina na wapiganaji mashujaa wa upinzani wao, na kusisitiza kuwa Yemen itaendelea kuwa ngao ya taifa katika kukabiliana na nguvu za uvamizi na wadukuzi wao.

Taarifa hiyo ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha jitihada za basiji na kuendelea kushikamana na mipango ya mafunzo na uwezeshaji, na kwa wakati mmoja kuonesha utayari kamili wa kutekeleza maagizo ya sayyid Abd al-Malik Badreddin al-Houthi, kiongozi wa Yemen, katika hatua zote zinazofuatia na kuendelea kwa mapambano na kuungwa mkono dini, taifa na walionyang’anywa haki popote walipo.

Mandhari hizi za uwanja katika mikoa ya Amran, Rima, Hajjah, Ma’rib, al-Mahwit, Ta‘iz na al-Bayda zinathibitisha kuendelea kwa harakati za umma wa Yemen, zinadhihirisha uaminifu kwa mashahidi na kuongezeka kiwango cha utayari wa kukabiliana na mpango wowote wa uvamizi, huku msaada wao wa kudumu kwa watu wa Palestina na wapiganaji mashujaa wao ukiongezeka, na ni ujumbe wazi ulimwenguni kwamba; Wayemeni wamejikita katika misingi yao na wako tayari kwa vigezo vyote vya kutetea dini, ardhi na hadhi yao.

Mwisho wa taarifa.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha